Leo Decemeber 31, 2017 makanisa 150 ya kanisa Katoliki yamewataka waumini wao kuitikia wito wa kuandamana wakiwa na biblia mkononi ili kushinikiza kutekelezwa kwa makubaliano yaliyotiwa saini mwaka mmoja uliopita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wasiwasi wa kukosekana utulivu katika nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia kanisa Katoliki lenye ushawishi Congo kuitisha maandamano ya amani yenye lengo la kurejesha uthabiti nchini humo ikiwa ni pamoja na kumtaka Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani.
Hakuna mtu yoyote kati ya Baraza la Maaskofu nchini humo au mwakilishi wa serikali ya mjini Vatican ambaye amezungumzia lolote kuhusiana na maandamano hayo.
Gavana wa mji huo Andre Kimbuta amesema kuwa maandamano hayo yasiyo na kibali hayawezi kuendelea kwa maelezo kuwa mji huo hauna maafisa wa polisi wa kutosha kusimamia maandamano ya leo.
Hata hivyo msemaji wa waratibu wa maandamano Leonie Kandolo amesisitiza kuwa licha ya kauli hiyo ya serikali maandamano yatafanyika na kuwa maafisa wa polisi wanalazimika kutimiza wajibu wao kuwalinda raia na mali zao.
Waandaaji wa maanadamano wametoa mwito kwa waumini kukusanyika baada ya misa ya asubuhi kwa ajili ya kushiriki maandamano hayo leo.
“TUSIKAE KIMYA TUKIONA HATUTENDEWI HAKI” – HUSSEIN BASHE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA