Mkurugenzi wa Tafiti Kutoka Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira(NEMC) Dr. Menani Jangu amesema miongoni mwa faida za uchakataji wa taka ni kupunguza uchafu katika dampo na utengenezaji wa mbole ambazo zinaathari ndogo kwa mazingira .
Hayo Ameyasema leo wakati wa uzinduzi mdogo wa kiwanda cha kuhifadhi mbolea na Kuzalisha Nzi huku akisema kwani kumekuwa na faida nyingi kama utengenezaji wa chakula cha wanyama ambacho kina nafsi kubwa katika kusaidia sekta ya mifugo .
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa kampuni ya bia ya Tanzania TBL Jose Morgan na Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya chanzi Andrew Wallace wamesema programu hiyo inatekelezwa nchini ikiwa ni sehemu ya kampuni ya bia katika kutoa mchango wake kwa jamii katika uhifadhi wa mazingira hususani kudhibiti taka za majumbani ambazo zimekua zikizalishwa kwa wingi katika majiji makubwa ikiwemo Dar es Salaam .
Naye msimamizi mkuu wa mradi huo Bw. Nicko Nyamanga amesema kupitia programu hiyo wataweza kuchangia pa kubwa katika kupunguza taka pamoja na kuzalisha protini kwa wingi kupitia inzi wanaotokana na taka hizo hivyo kusaidia kutatua changamoto za upungufu wa protini nchini .
Hata hivyo Kampuni hiyo imengia makubaliano baina ya kiwanda cha chanzi na taasis ya ab inbev ambayo pia ina unda kampuni ya bia ya Tanzania TBL ambapo ajira zaidi zikitegemewa kupewa kwa Wanatanzania huku asilimia 36 ya ajira hizo ni wanawake .