Uzinduzi huo rasmi wa kampeni ya “Maisha ni Hesabu’ unayolenga kuleta mapinduzi kwenye huduma za kibenki kwa makampuni kupitia ubunifu endelevu yenye kurasmisha ukuaji wa benki na kuonyesha mbinu zenye tija zinazolenga kuleta mapinduzi katika huduma za kibenki hasa kwa makampuni lilifanywa na NCBA Bank siku ya jumatano.
Akizungumza na waandishi wa habari , Ndg. Claver Serumaga, Mkurugenzi Mtendaji wa NCBA Bank Tanzania, alidhihirisha msisimko na matarajio yake na kusisitiza umuhimu wa kuwa na safari yenye mabadiliko.
Alisema, “Leo tunaingia katika safari yenye mabadiliko, tukiongozwa katika misingi ya “Maisha ni Hesabu”. Kampeni hii inalenga kuwajulisha waTanzania kwamba NCBA Bank ipo tayari kuhakikisha wanayafikia malengo yao.
NCBA Bank inaamini kwamba kila siku mfanyabiashara anafikiria kuhusu mahesabu yake, kama kuongeza vitendea kazi vyake, bidhaa zake, kuvuka mipakana kutanua biashara yake. Hayo yote ni kufikia malengo take Hivyo NCBA inaamini malengo yake ni mahesabu yake na sisi ni taasisi ya fedha inayohakikisha Hesabu zako zinatimizwa.
Ujumbe mkuu wa kampeni hii unaelezea kwamba namba ama hesabu zina maana kubwa sana katika ulimwengu wa kibiashara. Kila namba, kila tarakimu ina mchango wake katika mafanikio ya mbeleni. Ndg. Serumaga alikazia, “Tunafahamu kwamba namba zako ni zaidi ya tarakimu; ni uti wa mgongo katika utendaji wako, mapigo ya moyo katika biashara yako. Na hii ndiyo sababu tumejiandaa vilivyo kuhakikisha unafikia mafanikio, ambayo ndiyo nguzo ya malengo yako ya kifedha.
Alimaliza kwa kusema ,Kampeni ya “Maisha ni Hesabu” inahamasisha wafanyabiashara kuwa na fikra mpya kwenye mfumo wao wa kifedha na kuangalia ni jinsi gani namba zina nguvu za kupeleka biashara zao mbali zaidi. Wakiwa na NCBA Bank Tanzania, wafanyabiashara hawatakuwa tu na taasisi ya kifedha, bali mshirika sahihi, mwenye Mawazo ya mbali aliyejikita katika kuendeleza na kutimiza ndoto zao za kiuchumi.