Baada ya Jumamosi ya August 13 2016 kuchezwa michezo saba ya Ligi Kuu England, Jumapili ya August 14 2016 ilikuwa ni zamu ya kushuhudia wakongwe wa TOP Arsenal wakiwakaribisha Liverpool katika uwanja wao wa Emirates kucheza mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017.
Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa Emirates wamekubali kipigo cha goli 4-3, licha ya kuwa na rekodi nzuri dhidi ya Liverpool kwa mechi zao 10 za mwisho walizowahi kukutana, Arsenal kwa takwimu ya mechi zao 10 za hivi karibuni walizowahi kucheza dhidi ya Liverpool walikuwa wameshinda mara 5, kupoteza moja na kutoka sare mechi 4.
Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani ndio walianza kupata goli la uongozi dakika ya 31 kupitia Theo Walcott.
Baada ya hapo mchezo ulikuwa wa Liverpool kupachika magoli kupitia kwa Philippe Coutinho 45 na 56, Adam Lallana dakika ya 49 na Sadio Mane dakika ya 63, baada ya hapo Arsenal walijaribu kusawazisha lakini waliambulia kupachika goli mbili pekee kupitia kwa Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 64 na Calum Chambers dakika ya 75.
-
AFC Bournemouth 1 – 3 Manchester United
https://youtu.be/fOYUanaDVuw
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0