Papa Francis, siku ya jumapili amesema Vatican ipo tayari kusaidia kuwezesha kurejea kwa watoto wa Ukraine waliopelekwa Russia wakati wa vita.
Amesema Holy See tayari imesaidia kupatanisha baadhi ya mabadilishano ya wafungwa na itafanya kila linalowezekana kibinadamu kuziunganisha familia.
Ishara zote za kibinadamu husaidia, na ishara za ukatili hazisaidii, alisema Papa Francis, wakati wa mkutano wa wanahabari akiwa kwenye ndege akielekea nyumbani akitokea Hungary.
Francis pia alifichua mipango ya siri ya amani ambayo imekuwa ikiendelea.
Hata hivyo, hakutoa maelezo yoyote alipoulizwa iwapo alizungumza kuhusu mipango ya amani wakati wa mazungumzo yake mjini Budapest wikendi hii na Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, au mwakilishi wa Kanisa la Orthodox la Russia nchini Hungary alisema yupo tayari kufanya chochote kufanikisha hilo.