Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesitisha ziara yake iliyokuwa ikiendelea mkoani Dodoma katika wilaya ya Chemba na kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya kuwafariji na kufuatilia tukio la ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere.
Ajali ya Mv Nyerere imetokea jana majira ya mchana,baada ya kivuko kuzidiwa uzito wa watu na mizigo na kupinduka.Ambapo mpaka sasa watu 125 wameripotiwa kupoteza maisha na 37 kuokolewa wakiwa katika hali mbaya.
HUZUNI: Miili inaelea, maiti 125 zimtolewa majini, Helicopter ziko hewani