Binti mmoja mzaliwa wa Misri ajulikanaye kama Eman El-Deeb amefanyiwa mahojiano na shirika la utangazaji la BBC na kueleza kuwa ilimlazimu ahame nchini Misri kwa sababu ya nywele zake.
Eman El-Deeb ambaye nywele zake ni za kujisokota (curly) aliamua kuhamia nchini Hispania ambako ndiko anaishi hadi leo baada ya kugundua watu wengi Misri walikuwa wakikerwa na nywele zake.
Eman ambaye ana umri wa miaka 26 anaeleza kuwa mara nyingi aliambiwa na watu tofauti tofauti kuwa azinyooshe nywele zake jambo lililomkwaza hivyo akaamua ahamie sehemu ambayo aliamini atakuwa na amani.
“Uamuzi wa kuhama ulikuwa mgumu sana kwangu, sikuwahi kudhani nitahama nchi lakini nilikuwa nimechoka na nilifikia hatua ambayo nilitaka kuishi sehemu ambayo muonekano wangu hautamsumbua yeyote.” – Eman El-Deeb
Ridhiwani na Mama yake walivyocheza ‘Nani kama Mama’