Serikali ya Burundi imepiga marufuku matangazo ya mashirika ya utangazaji ya kimataifa ya BBC na VOA nchini humo kwa kipindi cha miezi sita kutokana na kinachodaiwa kuwa ni ‘kukiuka maadili ya kikazi’.
BBC imeingia kwenye ‘adhabu’ hiyo baada ya kinachoelezwa kuwa ni ‘kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo’.
Burundi sio nchi pekee kufanya hivyo, Jamruhi ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) pia imesitisha shughuli za utangazaji wa mashirika ya kimataifa nchini humo.
MCT wafunguka kuhusu zuio la mahakama dhidi ya sheria za habari