Mwito huo umetolewa Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 13, 2022 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha mbalimbali ya injili nchini, Alex Msama wakati akitambulisha Tamasha la Maombezi kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan na Taifa kwa Ujumla.
Msama amesema Tamasha hilo ambalo litahusisha Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa Ndani na Nje ya Nchi, limelenga kuiweka Tanzania kwenye maombi pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Tunajua Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ni Mchapakazi na amejitoa kwa ajili ya Kuwatumikia Watanzania, kwa hiyo Dhamira ya Tamasha hili ni Kufanya Maombezi kwa ajili ya Kumuomba Mungu aweze kumfanyia wepesi Rais wetu kwenye Utekelezaji wa majukumu yake ya Kila Siku kwa ajili ya Watanzania” amesema Msama.
Ameongeza kuwa Tamasha hilo la Maombezi limepangwa Kufanyika Jijini Mwanza November 11, 2022 ambapo litaendelea kwenye mikoa mingine hapa nchini.
Kwa Upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Emmanuel Mabisa amesema mpaka Sasa Maandalizi mbalimbali yamekamilika kwa Kuzungumza na Wachungaji pamoja na Maaskofu mbalimbali kushiriki Tamasha hilo la Maombezi kwa ajili ya Taifa.
“Tayari Wachungaji na Maaskofu mbalimbali wamethibitisha kushiriki kwenye Tamasha hilo kwa ajili ya Kupiga maombi kwa ajili ya Rais Wetu na Taifa kwa Ujumla kwa maana yatakuwa ni maombi ya Kitaifa” ameeleza Mabisa.