Baada ya mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Copa America kati ya Chile dhidi ya Colombia kusimama kwa zaidi ya saa moja, hatimae uliendelea na kupatikana kwa mshindi atakayecheza mchezo wa fainali dhidi ya Argentina Jumapili ya June 26 2016 katika uwanja wa MetLife.
Colombia licha ya mchezo kusimama na wao kupata nafasi ya kupumzika vya kutosha na kushauriana, walishindwa kuchomoa goli 2-0 zilizokuwa zimefungwa kipindi cha kwanza dakika ya 7 na Charles Aranguiz na Jose Fuenzalida dakika ya 11.
#MillardAyoUPDATES #LiveMatch #FullTime #Colombia 0-2 #Chile (#Aranguiz 7′ #Fuenzalida 11′) #CopaAmerica pic.twitter.com/Z394A6qO3V
— millard ayo (@millardayo) June 23, 2016
Argentina atacheza na Chile katika fainali lakini nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wa Copa America anapewa Argentina kutokana na rekodi yao ndani ya miaka 106 Argentina kapoteza mechi 7 peke dhidi ya Chile, wakati Argentina amewahi kumfunga Chile kwa zaidi ya mara 40.
Magoli yalioipeleka Chile fainali ya Copa America 2016
https://youtu.be/s8SJg51J5D4
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE