Leo April 11, 2018 Kijana Silidion Silvester mwenye umri wa miaka 31 aliyekuwa mkazi wa mtaa wa Kisindi kata Kashai mkoani Kagera amejinyonga hadi kufa baada ya kwenda na Mke wake kupima na kukutwa ameathirika peke yake na UKIMWI.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa mtaa wa Kisindi, Victor Nshange amesema kuwa leo asubuhi majira ya saa mbili alipewa taarifa na Dereva bodaboda kuwa kuna mtu amejinyonga ikamlazimu kufika eneo la tukio ili kujiridhisha.
Majirani wa maeneo hayo wamesema juzi marehemu alienda na mke wake kupima afya wakakuta Silidioni ameathirika hivyo ndani ya familia walishindwa kuelewana na Mke wake akaamua kuondoka hivyo yawezekana ndo maana amechukua maamuzi hayo.
Mtoto anaishi kwa kunywa uji kwa miaka mitano, ananyweshwa kwa Sindano