Hivi ni vipande vya video ya wimbo ambao umefanywa na wasanii 19 kutoka Africa ambao walikutana South Africa kwa ajili ya kampeni ya Do Agric ambao ni mradi kutoka One Campaign wimbo huo unaitwa Cocoa na Chocolate,miongoni mwa Madj walienda kushuhudia uzinduzi huo ni pamoja Dj Fetty kutoka Clouds Fm.
Kampeni hiyo ni kwa ajili ya kuhamasisha kilimo kwa vijana na wasanii wamekutana Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya uzinduzi wa video hiyo ambao unafanyika leo March 31,zaidi ya wasanii 19 kutoka katika nchi mbali mbali Africa wakiwemo Diamond (Tanzania) D’Bhanji na Femi Kuti (Nigeria), Fally Ipupa (DRC) na wengine wengi.
Video hiyo imekamilika na muda wowote kuanzia leo March 31 itaanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni.
Hivi ni vipande vya video hiyo.