Chelsea imethibitisha kumsajili Renato Veiga kutoka FC Basel kwa mkataba wa miaka saba.
The Blues wamelipa kitita cha Euro 14 milioni (£11.8m) kwa ajili ya kijana huyo, huku kukiwa na chaguo la kuongeza mkataba wake wa mwaka mmoja zaidi, ambao unaweza kumuweka klabuni hapo hadi 2031.
Veiga alijiunga na Basel mnamo Agosti 2023 kwa mkataba wa miaka minne, na akaimarisha nafasi yake katika kikosi cha kwanza baada ya kucheza mechi yake ya kwanza Septemba.
Aliendelea kucheza mechi 26 katika mashindano yote, akifunga mara mbili kwenye Ligi Kuu ya Uswizi.
“Nina furaha sana kuwa hapa,” Veiga aliviambia vyombo vya habari vya Chelsea. “Hii ni moja ya klabu kubwa nchini Uingereza – kubwa zaidi kwangu – na nina furaha sana kuanza.”
Veiga ni mchezaji wa tano kusajiliwa na Chelsea katika dirisha hili la usajili, akiwafuata Tosin Adarabioyo, Omari Kellyman, Marc Guiu na Kiernan Dewsbury-Hall ndani ya klabu hiyo.