Taarifa kutoka Uganda ni kwamba Maafisa wanne wa Serikali ya Uganda hivi karibuni wamesimamishwa kazi kutokana na madai ya kutoa takwimu za uongo juu ya wakimbizi wa nchini humo.
Uchunguzi juu ya wafanyakazi hao unaendelea, mmoja kati yao akiwa ni Kamishna wa Wakimbizi nchini humo Apollo Kazungu na uchunguzi huu pia utaangalia kama viongozi wa mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa walihusika.
Inaelezwa kuwa wafanyakazi hao walizidisha takwimu za idadi ya wakimbizi hao. Inasemekana kuwa Uganda ilichukua wakimbizi hadi milioni 1.4 kutoka Sudan Kusini na DRC ikiwa ni idadi ya juu zaidi kuliko nchi yoyote kwa mwaka 2016.
Alichozungumza Kibatala baada ya Sugu kuachiwa, ametaja kilichokuwa kinakwamisha dhamana
TATU MZUKA: Kitu amefanya Mshindi wa Mil 22 baada ya Kuipokea pesa yake