Mtu wangu wa nguvu najua kila Alhamisi nimezoea kukuletea picha za utoto za mastaa wa soka wa dunia, ila Alhamisi ya August 18 2016 naomba nikusogezee video ya miji waliokulia mastaa 15 wa dunia ambao wengi wetu tumezoea kuwaona katika mafanikio yao katika vilabu vya Ulaya.
Leo naomba nikuletee miji ya mastaa wa soka kama Lionel Messi aliyezaliwa Rosario Argentina, Zlatan Ibrahimovic aliyekulia Malmo Sweden, wengi wao tumewahi kusikia historia zao kuwa hawakutokea katika familia zenye maisha mazuri ila video inaonesha mitaa yao ilivyokuwa kwa sasa na baadhi zamani pia.
GOAL AND HIGHLIGHTS: Yanga vs MO Bejaia August 13 2016, Full Time 1-0