Mwanaume mmoja ambaye anatajwa kuwa Mwenyekiti la Baraza la Parokia nchini Ujerumani anaripotiwa kumng’ata mbwa ili kumwokoa paka mdogo aliyekuwa akishambuliwa na mbwa huyo.
Inaelezwa kuwa paka huyo alikuwa ni wa mwanaume huyo ambaye anafahamika kwa jina la Anthony Gabbott ambaye aliamua kupigana na mbwa huyo.
Gabbott anaelezwa kuwa alikuwa akipigana na mbwa wawili kwa wakati mmoja, na tukio hilo limemuacha amevunjika mkono wa kulia wakati anampiga ngumi mbwa mmoja huku akiwa anamng’ata mwingine.
Paka huyo ambaye alikuwa amepewa jina la dougie anaripotiwa kujeruhiwa vibaya usoni huku mbavu zake zikiwa zimevunjika.
Ahadi aliyoitoa Jebra Kambole akichaguliwa kuchukua nafasi ya LISSU