Ikiwa leo March 8, 2018 maadhimisho ya Siku wa Wanawake Duniani yakiendekea, kutoka nchini Burundi inaelezwa kuwa wanawake na wasichana zaidi ya 500 wa nchi hiyo wameuzwa katika biashara watu kwenda nchi za Uarabuni.
Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka ya shirika la kutetea haki za binadamu la ONLCT nchini Burundi, wanawake na wasichana hao wanapelekwa zaidi kwenye nchi za Oman, Saudi Arabia, Kuwait na Lebanon.
Uchunguzi ambao umefanywa na shirika hilo umebaini ya kuwa wanaojihusisha na biashara hiyo ya watu huwauza kwa hadi Dola za Marekani 1000 sawa na Shilingi za Tanzania Milioni 2.4 kwa kila mwanamke au msichana mmoja.
RPC Iringa amefunguka juu ya Abdul Nondo “Tutamshughulikia kama wahalifu wengine”