Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameendelea na ziara yake jijini Dar es salaam na leo ni siku ya nne . Jana alipokuwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Temeke alizungumza kuwa…..>>> ‘Pale mkoani ofisini kwangu nina wasaidizi 120 lakini ambao ninaweza kujivunia ni wanne tu, wengine wote ni mizigo’.
'Pale mkoani ofisini kwangu nina wasaidizi 120 lakini ambao ninaweza kujivunia ni wanne tu, wengine wote ni mizigo' -RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
Baada ya kauli hiyo kuleta mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, leo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Mbande Temeke, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amesema…….
>>>Tunalipwa fedha nyingi sana kuwahudumieni ninyi wananchi lakini ukienda hospitalini, polisi, ardhi utakutana na changamoto, najiuliza hizi changamoto zinatoka wapi kama watu wanatimiza wajibu wao, maana yake ni kwamba kuna watu wanakula mshahara ambazo ni kodi za wananchi na hawafanyi kazi yao’
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
VIDEO: ‘Nikikuta mgambo kituo cha polisi nitakula sahani moja na Sirro’-RC Makonda