Wizara ya Afya Tanzania imesema imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa Covid 19 Tanzania, hii ni kutokana na taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu na mwingiliano wa Watu wa Tanzania na Watu wa Nchi jirani na Mataifa mengine Duniani katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
“Tunakuwakumbusha Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19, na tahadhari hii ya leo ni kutokana na hali ya mwenendo wa ugonjwa wa Covid 19 Duniani na ongezeko la maambukizi Afrika zikiwemo Nchi jirani ambazo zimekumbwa na wimbi la tatu la mlipuko wa Covid 19 na maambuki yameongezaka maradufu kuliko ilivyokuwa katika wimbi la pili”
“Kwa mujibu wa taarifa kutoka WHO iliyotolewa katika jarida la wiki ya 24 inayoanzia June 07 hadi June 13, 2021 katika Kanda ya Afrika idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeka kwa wiki tano mfululizo “
“Mfano katia Wiki moja iliyopita Afrika Kysini, Uganda, Zambia, DRC, Namibia, Angola n.k zimeendelea kuonesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa isiyoshuka huku ikiripotiwa Nchi hzio kukumbwa na anuai ya virusi vipya vinavyosababisha Covid 19 kuwa kali zaidi na kuathiri hata mkundi ya wenye umri mdogo” ———-Mkurugenzi wa Idara ya Kinga – Wizara ya Afya, Dkt. Leonard Subi