Asubuhi ya Novemba 29 imetokea ajali ya Basi namba T178 DVB kampuni ya Ally’s Star baada ya kugonga kichwa cha Treni chenye namba V951 9006 kilichokuwa kikitokea stesheni ya Aghondi kuelekea manyoni kwenye makutano ya reli na barabara na kusababisha vifo vya watu 13 (wanawake 6 na wanaume 7) na majeruhi 25.
Naibu Waziri wa mambo ya Ndani ya nchi Jumanne Sagini amefika Manyoni na amewatembelea majeruhi waliopo hospitali ya Manyoni Mkoani Singida.