Wakazi wa Mapinga Bagamoyo, Boko na Bunju wamepaza sauti kwa pamoja kuomba Jeshi la Polisi kuongeza mbinu za kudhibiti wizi uliokithiri siku za karibuni wa vifaa vya magari kwenye maeneo hayo ambao umekua ukiwatia hasara na kuwarudisha nyuma kimaisha.
Wakazi hao wamepaza sauti baada ya tukio jingine lililotokea Mapinga Centre kwa Kibosha Wilayani Bagamoyo ambapo Wezi wameingia kwenye nyumba ya Mkazi mmoja na kuinyofoa vifaa mbalimbali vya gari aina ya IST na kumsababishia hasara ya shilingi milioni nne.
“Huyu Mtu aliamka asubuhi akaikuta gari imebaki fuvu tukaripoti Kituo cha Polisi Mapinga na kugundua kuwa hii ishu ina-trend sana maeneo ya Boko, Bunju na Mapinga, tunachojaribu kufanya ni kimoja sababu kwenye camera za CCTV kuna sura za Watuhumiwa zinaonekana tunaomba Watu watusaidie kuwapata”