Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya amewaagiza TAKUKURU kuwafanyia uchunguzi Wasimamizi wa ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Litola, baada ya Wasimamizi hao kufanya ubadhilifu wa zaidi ya Tsh. milioni 10 na kughushi sahihi za Watu kuwa wamepokea vifaa vya ujenzi wakati vifaa havijapokelewa huku Mzabuni akiwa tayari ameshalipwa.
Wasimamizi hao wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya Shule za Msingi (BOOST) wamehojiwa, baada ya Afisa Takwimu Linda Mapunda kughushi nyaraka na kumlipa mzabuni fedha za mabati 200, gypsum board pamoja na misumari kwa ajili ya kumalizia mradi huo.
DC Ngollo Malenya ameagiza Watu hao wahojiwe na kuanza uchunguzi mara moja na kuwafikisha Mahakamani wahusika uchunguzi ukikamilika huku akiwaasa Watumishi kuwa waadilifu na kuwaonya waachane na 10% ambayo itawaingiza matatani.