Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa na kuhojiwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa afisa Manunuzi na ugavi wa halmashauri ya Wilaya ya Hai Sabiano wambura.
DC Sabaya amefikia uamuzi huo baada ya afisa ugavi huyo anatuhumiwa kushindwa kupeleka vifaa vya ujenzi katika kituo cha Afya ambapo serkali kuu ilitoa Tsh milioni 30 toka mwaka jana mwezi wa nane (April 2019) kitendo ambacho kimepelekea kushindwa kukamilika kwa ujenzi huo.
Sambamba na hilo mkuu huyo wa wilaya amemuelekeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuchukua hatua ya kinidhamu ikiwepo kumsimamisha kazi wakati hatua za uchunguzi wa tuhuma za kuchelewesha kupeleka vifaa kwa wakati zikiendelea kuchunguzwa.
AUDIO: WEMA AMLILIA MGONJWA WA CORONA ALIEFARIKI “LALA PEMA ANKOO”