Imeelezwa kuwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando Jijini Mwanza kila mwaka inapokea zaidi ya Wagonjwa 200, wenye tatizo la uvimbe kwenye Ubongo.
James Lubulwa ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Ubongo, Uti wa mgongo pamoja na Mishipa ya fahamu ameeleza kwa sasa tatizo hilo linazidi kuonekana kutokana na kuongezeka kwa vifaa vya kufanyia vipimo (CT SCAN), ambapo Hospitali ya Bungando inakifaa cha kufanyia upasuaji mkubwa wa Ubongo OPERATING MICROSCOPE.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian Masaga amesema Upasuaji unaofanywa kwa Wagonjwa niwa Kibingwa kwani Hospitali hiyo ina Madaktari Wabobezi wazawa watatu na Madaktari wengine watatu kutoka nchini Marekani.