Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watuhumiwa waliowashambulia wapenzi wakiwa kwenye faragha wakidai kuwa wamewafumania.
Ametoa agizo hilo leo Agosti 6, 2021 jijini Dar es Salaam baada ya kuiona video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha kundi la watu wakiwavamia wapenzi hao na kuwadhalilisha.
Ayo TV imekusogezea video hii ya Waziri Simbachawene akizungumza kuhusu tukio hilo.
SHUHUDIA WABUNGE, WALIVYOUAGA MWILI WA ALIYEKUA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA