Mtu mmoja ambaye amefika katika kijiji cha Ngarash Wilayani Mondulu Mkoani Arusha amesema kwamba leo ni siku ya nne akiwa nyumbani kwa Hayati Edward Lowasa na Kazi yake amejitolea kufanya usafi na kula nyama tu na hajawah kula chakula kingine.
Akizungumza akiwa katika eneo hilo maarufu kwa kuchoma nyama amesema “Nashindia nyama tu hata wali sitaki,nipo hapa tangu jumanne nakula chakula sihitaji malipo yeyote nimetokea Arusha msiba ukimalizika naondoka”.