Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linawashikilia wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na kibali katika eneo la Kijiji cha Chemchem kata ya Mutuka wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.
Rcp mkoa wa Manyara Acp George Katabazi amesema tukio hilo limetokea July 13 Mwaka huu ambapo wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa kwa kutumia gari aina ya MARK X iliyokuwa ikitokea Arusha kwa kupitia barabara ya Babati “Baada ya kupata taarifa tuliweka mtego kwaajili ya kukamata gari hilo lakini Derera alivyogundua akachepusha gari kutoka Barabara kuu(Lami) na kuingia changarawe kuelekea Kijiji cha Chemchem ambapo ndipo tulipomkamata,upelelezi unaendelea na utakapokamilika watafikishwa Mahakamani ” Rpc Katabazi
Katika hatua nyingine katika Kijiji cha Kiongozi kata ya Maisaka Barabara kuu ya Arusha-Babati zimekamatwa dawa za kulevya aina ya mirungi bunda 264 sawa na Kilo 110 zikiwa zimehifadhiwa ndani ya magunia manne zikiwa zinasafirishwa na gari aina ya Noah likitoea Arusha kwenda Babati lakini baada ya dereva kuona anafuatiliwa alimama na kukimbia kusikojulikana huku juhudi za kumtafuta dereva huyo zikiendelea.
Rpc Katabazi ametoka wito kwa madereva na wamiliki wa magari kuacha kusafirisha madawa ya kulevya na wahamiaji haramu huku wananchi wakitakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kudhibiti matukio ya kihalifu na uhalifu.