Ester Maongezi mkazi wa kata ya Kimandolu Mkoani Arusha ambaye aliungua mkono wake wa kushoto kwa madai ya kuchomwa sindano kwenye duka la dawa alipokwenda baada ya kuambiwa ana ugonjwa wa UTI na kisha kukatwa vidole vyake vitano.
Ester amefikia hatua hiyo alipofikishwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru baada ya hali yake kuwa mbaya kutokana na vidole vyake kuanza kuungua.
Ester amesema afya yake ilianza kubadilika baada ya kuchomwa sindano na daktari kwenye duka hilo la dawa