Waziri MkuuKassim Majaliwa leo Septemba 2, 2023 amemkaribisha Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyopo Magogoni jijini Dar es Salaam na amemuahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kumteua Mheshimiwa Dkt Biteko awe Naibu Waziri Mkuu ili waweze kusimamia uratibu wa shughuli za Serikali. pamoja.
“…Kwa niaba yako Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu, tunakukaribisha hapa ofisini kwetu na tunakupongeza kwa kuaminiwa na mheshimiwa Rais kwa kupewa dhamana kubwa ya Naibu Waziri kwa lengo la kusimamia shughuli hizo. wa Serikali. Nawahakikishia kuwa mna timu imara ambayo inashirikiana wakati wote.”