Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dotto Biteko amesema haijailishi Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO, watakuwa na mipango ya namna gani lakini Watanzania wanataka umeme.
Dkt. Biteko amesema hayo leo September 13,2023 wakati akiongea na Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika la Umeme (TANESCO) kwenye Makao Makuu ya TANESCO, Ubungo Dar es salaam.
“Watanzania wanataka umeme, hata tungekuwa na mipango ya namna gani tukazungumza chochote tukaeleza kwa ufundi wa aina yoyote, mwisho wa siku Watanzania wanataka umeme, wanaweza wasijali mchakato wa Watanzania kupata umeme, sisi lazima tujali mchakato wa kuwapatia umeme”
“Jambo tunapaswa kufanya kama Wizara ya Nishati ni kuziunganisha Taasisi nyingine wezeshi za kuwafanya Watanzania wapate umeme ili lawama iwe ndogo kwa TANESCO umeme uwafikie Watanzania ili kazi ambayo Rais ametupa tuweze kuifikia na kazi hii hatuwezi kuifanya kama tutachukua muda mwingi kudeal na personality badala ya ishu”
“Kuna Watu wana hofu ya mabadiliko na hofu hii tunaitengeneza sisi Viongozi kwasababu ukiingili mahali badala ya kushughulika na jambo unaanza kushughulika na Watu”