Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza Kijana Majaliwa Jackson aliyehusika kuwaokoa Watu 24 kwenye ajali ya ndege iliyotokea Bukoba siku jana atafutiwe kazi kwenye Jeshi la Uokozi.
Agizo hilo lililotolewa na Rais Samia kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambapo ameagiza Kijana Majaliwa Jackson akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na atafutiwe nafasi kwenye Jeshi la Uokozi ili Kijana huyo apate mafunzo zaidi kutokana na ujasiri wake huo kisha aingie kwenye Jeshi hilo ambalo linahitaji ujasiri aliouonesha.
Muda mchache baada ya agizo hilo video Fupi iliyosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii imemuonesha kijana Majaliwa Jackson akisindikizwa na polisi mpaka kwenye gari ya polisi tayari kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Samia kwa kijana Majaliwa Jackson kujiunga na jeshi la Uokozi nchini.