Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Shinyanga kwa kiwango cha lami wenye urefu wa kilometa 2.2 ni moja ya mikakati ya Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani, kwa kuboresha mtandao wa safari za anga ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji.
Ujenzi wa uwanja huo utaanza kutumika tarehe 3 Octoba 2024 na pindi utakapokuwa umekamilika utakuwa na uwezo wa kupokea ndege za ukubwa wa Q400.