Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama ya moyo na mishipa ya damu, figo, saratani, kifua sugu, kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi kama vile ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell Disease).
Ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanaua watu zaidi ya milioni moja kila mwaka – na mtu yeyote anaweza kuupata.
Husababishwa wakati mwili hauwezi kuchakata sukari (glucose) yote katika mfumo wa damu; matatizo yake yanaweza kusababisha mshtuko wa moyo, kiharusi, upofu, figo kushindwa kufanya kazi na kukatwa kiungo cha chini.
Kuelekea siku ya kisukari Dunia inayotarajiwa kufanyika tarehe 14 Novemba mwaka huu, Daktari Bingwa wa magonjwa ya kisukari dkt Maneno Mlawa akizungumza na waandishi wa habari Jijini dar es alaam amesema kuwa maadhimisho ya mwezi huu yanalenga kuongeza ufahau juu ya ugonjwa huu na kuelimisha jamii namna ya kujiepusha mapema kutokana na ugonjwa wa kisukari.
Kauli mbinu ya mwaka huu ni ufikiaji wa huduma ya kisukari kwani mamilini ya watu wanakosa huduma stahiki za ugonjwa wa kisukari
Tazama zaidi….