Baada ya kukithiri kwa matukio ya moto katika Shule mbalimbli nchini Jeshi la Polisi kupitia mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai DCI Camillius Wambura amewaomba Wakuu wa Shule kushirikiana na Wakuu wa Vituo vya Polisi kutoka maeneo yao kuimarisha Ulinzi katika maeneo ya Shule zilizo na mwingiliano na Jamii.
DCI Wambura ameiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI kufuatilia mifumo ya umeme katika Shule mbalimbali Nchini.