Maandamano yenye ghasia yameendelea nchini Afrika Kusini usiku kucha juu ya kufungwa jela kwa Rais wa zamani Jacob Zuma na kufanya uharibifu wa mali mbalimbali.
Duka moja kubwa huko Pietermaritzburg, katika Mkoa wa KwaZulu-Natal limechomwa moto leo Julai 12,2021 sambamba na uporaji na uharibifu wa mali ukiendelea.