Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh. Bil 100 baada ya kushinda shauri lililofunguliwa na familia ya Bw.Valambia huko nchini Marekani kwa madai ya kutoridhika na mkataba wa kibiashara walioingia kati ya familia hiyo na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Wakili wa mkuu Serikali Gabriel Malata wakati wa mafunzo ya mawakili wa Serikali yaliofanyika mjini Morogoro ambapo amesema kuwa familia hiyo ilifungua kesi hiyo kwa madai ya kutoridhika na mkataba walioingia na Serikali ya Tanzania.
IFAHAMU MAANA YA JINA LAKO NA ANAYEFAA KUWA MUME/MKEO “MAJINA MENGINE YANAKATAANA, MAAJABU 18”