Gloomy Sunday (Jumapili ya Huzuni) ni wimbo uliotungwa na Rezso Seress (Rudi Spitzer), msanii kutoka nchini Hungary mwaka 1933. Reszo alitunga maneno ya wimbo huo na kupiga mwenyewe ala ya huzuni ya wimbo huo, baada ya kuachwa na mpenzi wake
Inaelezwa kwamba kitendo cha kuachwa na mwanamke aliyekuwa akimpenda sana, kilimfanya apatwe na huzuni kali na msongo wa mawazo, na katika kipindi hicho ndipo alipopata wazo la kutunga mashairi na baadaye kuutengeneza wimbo huo.
Kwa sababu aliuimba akiwa na huzuni kali, wimbo nao ulijawa na hisia kali, za mtu anayelalamika kuvunjwa moyo na mpenzi wake, akifananisha kitendo cha kuachwa kuwa sawa na kufiwa na mpenzi aliyekuwa anampenda.idk_1.png
Awali ulionekana kuwa wimbo wa kawaida wa huzuni, lakini matukio ya watu kuyakatisha maisha yao baada ya kuusikiliza mara nyingi wimbo huo kwa kuurudiarudia yalianza kuripotiwa, wengine wakiacha kabisa ujumbe kwamba wamejiua baada ya kusikiliza wimbo huo
TAZAMA ZAIDI…