Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham amepokea Vifaa Tiba na Dawa vyenye thamani ya Milioni 300 kutoka Bohari ya Dawa Msd kwaajili ya vituo vya Afya na zahanati zilizopo wilayani humo.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo Meneja wa Msd Mkoa wa Dar es Salaam Betia Kaema amesema tayari Serikali imeshalipia dawa kwaajili ya vituo vya Afya na Zahanati zote nchi hivyo kwasasa wao kama Msd jukumu lao ninkusambaza dawa hizo kwa awamu ili kuhakikisha changamoto ya Vifaa tiba na upatikanaji wa dawa unapungua Nchi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe Salim Alaudin Hasham ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuhakikisha huduma za Afya zinaimarika nchi na Amewaomba Msd kuongeza kasi ya ugawaji dawa hizo na vifaa tiba kwani uhitaji ni mkubwa tofauti na idadi iliyopo katika mahospitali na Zahanati.
Vifaa tiba hivyo na Dawa vilivyokabidhiwa na Msd vitagawiwa katika kituo cha Afya cha Lupiro,Iragua na Mwaya pia Zahanati za Ruaha,Euga na Sali zitapata kwa awamu hii.