Zaidi ya vijana 1500 wameendelea kunufaika na Mradi wa Going Beyond kutoka mikoa mitatu ambayo Dar es Salaam Morogoro na Dodoma ikiwa ni lengo la kuhakikisha vijana wanaendelea kutumia mfumo wa biashara kidigtal
Akizungumza na waandishi wa Habari Emmanuel Richard Mahe Mwezeshaji wa Vijana amesema kuwa kwa kipindi cha miezi sita mradi wa Going Beyond umewafikia vijana zaidi ya 1500 na akiwataka vijana wengine pamoja na wajasiriamali kuendelea kujisajiri katika mradi huu
Aidha uwepo wa mradi wa Going Beyond unatajwa kuwasaidia wajasiriamali vijana pamoja na wanawake katika masuala ya biashara ikiwemo kutambua faida za usajiri wa biashara zao
Mwamvua Abdul ni miongoni mwa wanufaika wa mradi huu amesema kwa kipindi cha miezi sita aliyojiunga amepata faida kubwa ikiwemo kutambua umuhimu wa matumizi ya biashara kidgtal kwani kunaongeza kupata wateja katika biashara
Kwa upande wake Theresia Muna ameeleza sababu kubwa inayowafanya vijana wengi kushindwa ni kukosa uthubutu wa kuamua kufanya maamuzi ikiwemo kushiriki katika miradi ambayo inaweza kuleta faida kwao