Jumla ya Vijana 20 wamefikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa Akiwemo mfanya biashara Gulam Rasori kwa makosa mbali mbali ikiwemo la uhujumu uchumi kwa kutoboa bomba la mafuta Ghafi kutoka Tanzania kwenda Zambia ( TAZAMA ) na kusabababisha hasara ya zaidi ya bilioni 2.
Akisoma mashtaka yao mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Iringa Adelina Ngwaya amesema washtakiwa hao 20 wanakabiliwa na mashtaka 6 ikiwemo la kutoboa bomba la mafuta ghafi mali ya TAZAMA lililoopo eneo la Ruaha Mbuyuni mkoani Iringa kwa kutoboa chini kwa chini Ardhini na kuchepusha mafuta hayo lita zaidi ya laki saba ambapo watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi .
Amesema kati ya tarehe moja September 2023 mfanya biashara Ghulam na wenzake kwa makusudi na huku wakijua ni kinyume na sheria waliharibu kwa kutoboa na kuchota mafuta hayo
Kosa lingine walilosomewa wote ni kuongoza genge la uhalifu kinyume na kifungu cha 60 cha sheria ya uhujumu uchumi.
Kosa lingine ni kosa la utakatishaji fedha ambapo mtuhumiwa Aliyefahamika kwa jina la Miraji alijipatia piki piki yenye thamani ya shilingi milioni 1 na laki tatu huku akijua fedha hiyo ni ya utakatishaji.
Kosa lingine ni kwa mfanyabiashara Ghulam ambapo tarehe 10 alijipatia dizel lita zaidi ya laki 7 wakati akifahamu ni ya utakatishaji.
Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imehairishwa tena hadi Aprili 15 mwaka huu itakapo tajwa tena kutokana na mahakama kutokuaa na nguvu ya kisheria ya kusikiliza mashtaka ya uhujumu.