Zaidi ya vijana 2500 kutoka umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro wanatarajia kukutana na kufanya tamasha kubwa la kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta.Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Rais Wilayani humo kutoa fedha za miradi ya maendeleo.
Akizungumza na Waandishi wa habari katibu wa hamasa na chipukizi wilaya ya Ulanga Thomas Machupa amesema kushirikiana na Viongozi wa umoja wa Vijana chama hicho Wilayani Ulanga umeona kuna kila sababu ya kumshukuru Rais Samia kutokana na kuwajali vijana ikiwemo ujenzi wa Chuo cha Ufundi stadi (VETA) unaoendelea katika wilaya hiyo ,miradi ya elimu ,maji,afya na barabara.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ulanga Shahista Selemani amesema mgeni rasmi katika tamasha hilo anatarajiwa kuwa makamu mwenyekiti UVCCM Taifa Rehema Sombi pamoja viongozi mbalimbali wa serikali kutoka ndani na nje ya Mkoa Morogoro.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Katika Mji Wa Mahenge Makao makuu ya Wilaya ya Ulanga mnamo Juni 10 mwaka huu ikimbiatana na shughuli za kijamii ikiwemo kuona wagonjwa,wafungwa na kutembelea watoto yatima.