Urusi mnamo Jumatano (Aprili 3) iliripoti ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaotia saini kandarasi za kujiunga na jeshi la taifa hilo.
Kulingana na ripoti ya Reuters, ongezeko hili la idadi ya watu wanaojiandikisha kwa jeshi la Urusi linafuatia shambulio baya kwenye ukumbi wa tamasha karibu na Moscow mwezi uliopita na kuua takriban watu 144.
Kulingana na wizara ya ulinzi ya Urusi, zaidi ya watu 100,000 wametia saini mikataba tangu mwanzoni mwa mwaka. Kati ya hayo, takriban 16,000 wamejiandikisha katika siku 10 zilizopita pekee.
Katika taarifa, wizara hiyo ilisema kwamba wagombeaji wengi wa hivi majuzi walitaja hamu ya kulipiza kisasi waliouawa katika shambulio la Machi 22 katika ukumbi wa tamasha wa Crocus City Hall.
“Wakati wa mahojiano yaliyofanywa wiki iliyopita katika vituo vya uteuzi katika miji ya Urusi, wagombea wengi walionyesha hamu ya kulipiza kisasi kwa wale waliouawa katika mkasa uliotokea Machi 22, 2024 katika mkoa wa Moscow kama sababu kuu ya kuhitimisha mkataba,” ilisema. .