Mkuu wa gereza la mahabusu Mkoani Morogoro SP Nicodemos Tenge amewataka wanawake wote kuhakikisha wanawalinda vyema watoto wao na kuwalea vyema hususani katika kipindi hiki Cha ongezeko la sayansi na teknolojia ambayo huwafanya Vijana wengi kutenda Mambo ya yasiyofaa na wengine kuishia kufungwa jera
Ameyasema hayo alipokuwa akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa wanawake hawa ambao ni watumishi wa TANESCO Mkoani Morogoro
Aidha amewataka kuhakikisha wanasimama na familia zao kuwalinda kusimamia katika Imani zao kwani msingi wa mtu mzima huanza akiwa mtoto
Kwa Upande wake mwanasheria kutoka Gereza la mahabusu Mkoani Morogoro amewapongeza wanawake kwa Moyo walio ufanya kwa kujitoa kwaajiri ya wengine pia amewataka waondoe Imani ya kuwachukulia wafungwa kama watu ambao siku zote ni wakosaji.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa TANESCO Zuwaida Rwezauls ameeleza ni jinsi gani waliguswa na kujitoa ili kusaidia watu ambao wapo Magerezani
Zuwaida anasena kama Wanawake wa TANESCO wameona waungane na Wanawake wote duniani kwa kutoa msaasa katika gereza Hilo huku akitoa Wito kuwakumbuka Jamii hiyo kwani inatengwa na watu na kuona kama wenye makosa hawastahili msaada jambo ambalo sio kweli