Zaidi ya vijana 1000 kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa Morogoro wanatarajia kukutana pamoja kupata elimu ya Ujasiriamali pamoja na mbinu mbalimbali za kujiajiri Ili kujikomboa kwenye wimbi la umaskini na kuwa tegemezi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Morogoro Mkurugenzi wa Taasisi ya ufaulu project Simon Joseph amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na Tasisi ya Universal Career Development Pivot UCDP iliyopo Mkoani Morogoro amewataka Vijana wanaosoma vyuo vikuu kuzitumia fursa wanazozipata ili kujiondoa na wimbi la ukosefu wa ajira ambalo limekuwa kilio kikubwa kwa Vijana wengi.
Simon amesema wameandaa tukio maalum litakalowakutanisha zaidi ya Vijana 1000 huku dhima kubwa ni kuwakomboa na kuwaondoa katika wimbi la umaskini.
Kongamano Hilo litatambulika kwa jina la nje ya box youth talk hili linatarajia kufanyika tarehe 4/5/2024 chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro huku likitarajiwa kuhudhuriwa na watu maarufu akiwemo mtangazaji wa zamani BBC Salim Kikeke.
Kwa Upande wake Patrick Kawogo mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji UCDP Tanzania amewataka vijana kujitokeza kwa wingi siku hiyo lengo ni wao kuja kupata maarifa yatakayowasaidia Vijana kujikomboa kiuchumi
Kongamano hilo linatambulika kwa jina la Nje ya Box yenye lengo la kuhamasisha vijana kutengeneza fursa kujiajiri wanapohitimu masomo Yao ya vyuo vikuu badala ya kusumbilia ajira Serikalini.