Wanajeshi wa Israel walipigana vita vikali na Hamas kusini mwa Gaza siku ya Jumatano baada ya kufika katikati mwa mji wa Khan Younis, na kuwalazimu raia wa Palestina kutafuta hifadhi kwingine huku idadi ya maeneo salama ikipungua.
Ndege za kivita za Israel pia zilishambulia maeneo ya mwambao yenye wakazi wengi zaidi katika moja ya awamu kali zaidi za mapigano katika kipindi cha miezi miwili tangu Israel ianze kampeni yake ya kijeshi ya kulitokomeza kundi la Wapalestina.
Madaktari wa Kipalestina walisema hospitali zilikuwa zikifurika watu waliokufa na waliojeruhiwa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na vifaa vinaisha.
Mamia ya maelfu ya watu waliofurushwa kutoka kaskazini walikuwa wakitafuta hifadhi katika maeneo ambayo yanapungua kusini mwa Israel yaliyoteuliwa kama maeneo salama.
Baada ya kudhibiti kwa kiasi kikubwa eneo la kaskazini mwa Gaza, wanajeshi wa Israel na vifaru vilisonga mbele zaidi kusini na kumzingira Khan Younis kufuatia kusambaratika kwa mapatano ya siku saba wiki iliyopita.