Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jeshi la Wananchi Tanzania, Jeshi la Polisi na Zimamoto vimeungana kufanya matembezi na mazoezi ya viungo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma kwa lengo la kuimarisha afya za Askari hao.
Akizungumza na millardayo.com wakati wa mazoezi hayo Kamanda wa Kikosi cha Jeshi 24 Kigoma Leban Thomas amesema mazoezi hayo ya pamoja yatasaidia kuongeza ushirikiano katika kudhibiti vitendo vya uhalifu, huku washiriki wakisema kukutana pamoja kunaimarisha mahusiano kati yao katika utendaji kazi.