Mapigano ya silaha ya kuwania madaraka nchini Sudan yamekuwa yakiendelea tangu Aprili 15 kati ya vikosi vya jeshi na vya Radiamali ya Haraka. Maelfu ya watu wameuawa na mamia ya maelfu ya wengine kukimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo.
Hitilafu kati ya Abdul Fattah al-Barhan, mkuu wa Baraza la Utawala ambaye pia ni kamanda mkuu wa jeshi la Sudan, na Mohammad Hamdan Daghlo (Hamidati), kamanda wa vikosi vya Radiamali ya Haraka, zilijitokeza baada ya kusainiwa mkataba wa kuunda kipindi cha mpito na kukabidhiwa madaraka kwa raia.
Vikosi vya Radiamali ya Haraka vya Sudan vilitangaza jana Jumatatu kuwa vimefanikiwa kuiangusha ndege ya kivita ya jeshi la nchi hiyo.
Hakuna maelezo yaliyotolewa na jeshi la Sudan kuhusu madai hayo.
Kwa upande wa pili, vyanzo vya habari vimeripoti kuendelea mapigano makali kati ya jeshi na vikosi vya Radiamali ya Haraka vya nchi hiyo.
Wakati huo huo, raia watano wamepoteza maisha wakati kombora lilipolenga nyumba moja huko Omdurman, kaskazini magharibi mwa Khartoum.
Kamati za mapambano nchini Sudan pia zilitangaza Jumapili kwamba kuna watu 11 waliofariki, wakiwemo watoto wawili na mwanamke mmoja, katika uchunguzi wa hospitali moja ya mjini Khartoum.