Manchester United, Arsenal, Chelsea na Liverpool wote wako kwenye kinyang’anyiro cha kuwania saini ya Adrien Rabiot.
Mfaransa huyo ni mchezaji huru baada ya kuondoka Juventus na amevutia vilabu vikuu vya Ulaya, vikiwemo Galatasaray na Atletico Madrid, kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport.
Liverpool wanamtaka kiungo mpya na wameona dhamira yao ya kutaka kumsajili Martin Zubimendi ikiporomoka.
Arsenal, wakati huohuo, wako kwenye mazungumzo ya kumsajili Mikel Merino ili kuimarisha chaguo la Mikel Arteta na Erik ten Hag anajulikana kutaka kiungo mpya wa Man Utd – huku Manuel Ugarte wa PSG akihusishwa.