Mchezaji wa Manchester City Kevin de Bruyne na Mohamed Salah wa Liverpool wanaweza kuhamia Mashariki ya Kati.
Wachezaji kandanda kadhaa wamebadilishana soka la Ulaya na kujiunga na Ligi ya Saudia msimu huu.
Hii inajumuisha wachezaji kama N’Golo Kante wa Chelsea, Edouard Mendy, na Kalidou Koulibaly; Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson; Allan Saint-Maximin wa Newcastle; na mchezaji mwenzake wa City De Bruyne Riyad Mahrez.
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror la Uingereza, Wasaudi sasa wanawatolea macho Salah na De Bruyne, ambao wana mataji matano ya Ligi Kuu ya England na Tuzo tatu za Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA kati yao.
Mpango huo ni kuwarubuni wachezaji hao wawili katika dirisha dogo la usajili mwakani.
Salah na De Bruyne watakuwa na umri wa miaka 32 ifikapo majira ya kiangazi ya 2024 na wanaweza kuvutiwa na ofa nono zinazoonyeshwa na Wasaudi.