Msaidizi wa zamani wa muigizaji wa Marekani Vin Diesel anamshtaki nyota huyo wa Fast & Furious, akimshutumu kwa kumnyanyasa kingono wakati wa kurekodi filamu ya Fast Five ya mwaka wa 2010.
Wawakilishi wa mwigizaji huyo, jina halisi Mark Sinclair, hawakujibu ombi la BBC la kutoa maoni yao.
Asta Jonasson anadai katika kesi hiyo kwamba mwigizaji huyo alimbamiza ukutani huku akijichua.
Pia anashtaki kwa kufutwa kazi kimakosa, akidai kampuni yake ilimfukuza kazi saa chache baada ya shambulio hilo linalodaiwa.
Kesi ya Bi Jonasson, ambayo iliwasilishwa Los Angeles siku ya Alhamisi, inadai kwamba unyansaji huo wa kingono ulifanyika katika hoteli ya St Regis mjini Atlanta wakati wa kurekodi filamu ya Fast Five.
Anasema katika kesi hiyo kwamba Bw Sinclair, 56, alimshinda nguvu akiwa katika hoteli yake na kupuuza ombi la Bi Jonasson la kutoridhia huku akimpapasa.